Balozi wa Ujerumani Nchini Egon Konchake
Akizungumza na waandish wa habari jana jijini Dar es Salaam Balozi wa Ujerumani Nchini Egon Konchake alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa serikali kuwahudumia wakimbizi serikali yake imeamua kuungana na Tanzania kwaajili ya kuwasaidia wakimbizi hao.
Alisema kuwa Ujerumani itaendelea kulisadia shirika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi UNICEF na mashirika mengine ya kiserikali yanayotoa msaada kwa wakimbizi.
Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi Simba Yahya alisema kutokana na hali ya chakula kuwa mbaya mkoani Kigoma ambako wakimbizi wengi wapo, fedha hizo zitatumika kwaajili ya chakula na huduma nyingine za kijamii.