
Akiongea na East Africa Radio katika mahojiano maalumu, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema ujenzi wa barabara hiyo ni moja ya hatua za serikali inazoendelea kuchukuwa ili kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
Prof. Mbarawa amesema wizara yake inampanga kujenga barabara za juu za kupitisha magari tatu na zawaenda kwa miguu 4 ambapo wataanza na barabara ya Mwenge na maeneo mengine yatafuata.
Prof. Mbarawa amesema, wataalamu wanaendelea na kubaini maeneo mengine mapya ambayo barabara za juu zitajengwa katikati ya Jiji na kwamba ujenzi wa barabara hizo ni za muda mfupi wa miezi minne hadi sita na itagharimiwa na fedha za ndani.