Taarifa hiyo imetolewana Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni Mheshimiwa Mussa Natty, alipokuwa akizungumza kwa njia ya simu kwenye kipindi cha Supermix kinachorushwa na East Africa Radio, na kuleza kuwa mpaka kufikia mwezi january bara bara hiyo itakuwa kwenye hatua za ujenzi.
Mh. Natty amesema hivi sasa bara bara hiyo ipo kwenye mradi ulio chini ya benki ya dunia, hivyo mpaka mwezi Disemba itakuwa imeshapata mkandarasi na kuanza ujenzi wake.
"Kuna mpango mkubwa unaitwa Dar es salaam Metropolitan Develeopment Project, na mpango huu ni wa bank ya dunia, na kwamba barabara ya Simu 2000 ina urefu wa kilometa 1.8 kwa hiyo bara barahyo itajengwa chini ya mradi huo wa DMDP, sasa hivi watumiaji wasubiri mradi huo na tunategemea disemba tutapata kontrakta wa kuanza kufanya kazi, na ikichelewa sana ni Januari", alisema Mh. Natty..
Pamoja na hayo Mh.Natty amesema kwamba upande wa bara bara ya Makumbusho sokoni ambayo ina urefu wa kilomita 1.3, itagharimu shilingi bilioni 1.521 na haina fidia, na pia ujenzi utaanza hivi karibuni.




