
Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza, anayeshughulikia biashara na uwekezaji kwa Tanzania, Lord Hollick
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ubalozi wa Uingereza iliyotolewa kwa vyombo vya habari imesema ziara ya Hollick itasanifu ubora, uzoefu na ubunifu wa kampuni za Uingereza na atajikita kuangalia fursa zilizopo kwenye gesi, mafuta na miundombinu.
Katika ziara yake hiyo atakutana na wawakilishi wa Serikali ya Tanzania pamoja na kampuni za Uingereza zinazofanya kazi za uwekezaji nchini au kupanga kuangalia fursa na kuwekeza nchini.
Hollick katika vikao vyake na serikali ya Tanzania ataonesha namna gani utaalamu wa kampuni za Uingereza zinavyoweza kuchangia katika Tanzania ya viwanda na uwezeshaji wa kifedha kutoka UK Export Finance unavyowezesha mchakato huo mzima.
Hii ni ziara ya nne kwa mjumbe huyo kutembelea nchini na kwa mara ya pili ndani ya mwaka huu 2016 ikiwa ni ishara ya dhamaira ya Uingereza kuchochea biashara na uwekezaji nchini Tanzania.