Jumanne , 10th Feb , 2015

Takwimu zinaonesha kuwa kwa kila wasichana watano wanaoolewa kati yao wasichana wawili hawajafikia umri sahihi wa kuolewa wa ambao ni miaka 18

Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na watoto Sophia Simba amesema kuwa Takwimu zinaonesha kuwa kila wasichana watano wanaoolewa kati yao wasichana wawili hawajafikia umri sahihi wa kuolewa wa miaka 18

Waziri Simba ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa uwekaji saini mkataba wa kukomesha ukeketaji wasichana na ndoa za utotoni kati ya nchi ya Tanzania na Uingereza iliyowakilishwa na Balozi wao nchini Bi. Diana Melrose.

Hata hivyo Bi Simba ameongeza kuwa serikali imeanzisha njia za siri za kuwakamata wale wote wanaojihusisha na masuala ya ukeketaji.

Kwa upande wake mkurugenzi wa TAMWA Bi Valerie Msoka amesema kuwa sheria zilizopo kwa sasa hazifuatwi kutokana na jamii kubwa kutokuwa na muamko wa kuwalinda watoto wa kike