Jumatano , 9th Sep , 2015

Wakazi wa vijiji vya Chikola, Mpinga na Tulugano vilivyoko wilayani Bahi mkoani Dodoma wameitaka Wizara ya nishati na Madini kupeleka maofisa wake katika eneo hilo kufuatia kuwepo kwa taarifa za kugundulika kwa madini ya dhahabu.

Baadhi ya Wananchi wakiwa katika shughuli za Uchimbaji katika mgodi huo usio Rasmi

Eneo hilo la mgodi ambalo sio rasmi lipo katika mpaka wa vijiji hivyo ambapo kwa muda wa juma moja lililopita ilikuwa ni pori lakini mara baada ya kuwepo kwa taarifa za kupatikana kwa dhahabu limegeuka lulu kwa watu kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo mikoa ya kanda ya ziwa na kaskazini wanaoingia kwa makundi bila kufuata taratibu hali inayozua hofu ya uvunjifu wa amani na kuibuka kwa milipuko ya magonjwa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Chikola Peter Masaka akiwakilisha wenyeviti wezake amesema eneo hilo limepata baraka kutoka kwa uongozi wa juu wa wilaya ya Bahi kama anavyobainisha hapa.

Mfaume Jumanne ni mmoja kati wachimbaji waliofika eneo hilo akitokea mkoani Shinyanga na anaelezea matumaini yake ya kupata utajiri huku akiitaka serikali irasimishe sehemu hiyo kama eneo la mgodi wa wachimbaji wadogo.