Mkurugenzi wa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi.
Prof Janabi ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam, wakati wa utoaji wa huduma za kijamii One stop Jawabu katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke.
Prof. Janabi amesema kuwa ukuaji wa uchumi unafanya maisha kuwa rahisi kwa watu kuwa na uwezo wa kununua vyakula vya aina tofauti lakini pia utumiaji wa usafiri wa mara kwa mara yote ni sababu ya ukuaji wa magonjwa ya moyo.
“Kadri uchumi unavyokua na watu wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa hayo kwa sababu watu wanakuwa na fedha za kununua vyakula vingi sambamba na matumizi ya usafiri binafsi” amesema Prof Janabi.