Alhamisi , 5th Mei , 2016

Bunge limepitisha Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, kwa mwaka wa fedha 2016/2017, baada ya kufanyika kwa mjadala wa siku mbili ndani ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba.

Katika bajeti hiyo iliyopitishwa serikali imesema kuwa itahakikisha inatokomeza matumizi ya Jembe la Mkono hapa nchini na badala yake wakulima wajikite katika matumizi ye jembe la trekta ili waendeshe kilimo chenye tija.

Akizungumza mara baada ya kupitishwa kwa bajeiti hiyo Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa kwa sasa wamepanga kuonana na wafugaji wa wilaya zote ili kutatua kwanza Migogoro ya Ardhi.

Aidha, Mhe. Mwigulu amesema endapo kilimo kitaboreshwa katika aina ya ulimaji itaweza kuwa ajira kwa vijana wengi amba wengi wanakimbia kutokana na na sehemu kubwa kutumia jembe la mkono ambapo amesema watafanya mchakato wa upatikanaji wa matrekta kwa wakulima.

Mhe. Mwigulu amesema kuwa wataita kikao cha mawaziri wa wizara zinazohusika na Ardhi pamoja na Hifadhi ambazo ni sehemu kubwa wanahusika katika kuweza kutatua migogoro hiyo ya ardhi

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba