Jumanne , 3rd Mei , 2016

Serikali ya Tanzania imesema kuwa imeanza kuchukua hatua kadhaa katika kuhakikisha kuwa fedha za miradi ya maendeleo zinafika kwa wakati ili kuharakisha kukamilika kwa miradi ya maendeleo ambayo imekua haifikishiwi fedha.

Naibu wa Fedha na Mipango Mhe. Ashantu Kijaji

Akizungumza Bungeni Mjini Dodoma, Naibu wa Fedha na Mipango Mhe. Ashantu Kijaji, amesema hatua kadhaa zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kuongeza mapato ya ndani ya serikali ili kuongeza pato la serikali kwa ujumla.

Mhe. Kijaji alizitaja hatua hizo ni pamoja kubana na kuziba mianya ya ukwepaji kodi ili kuhakikisha kuwa kila anaestahili kulipa kodi analipa kodi stahiki na kupanua wigo wa kodi kwa kutafuta vyanzo vipya.

Aidha Naibu Waziei huyo alitaja hatua nyingine ni kuweka mazingira wezeshi kwa mlipa kodi ili aweze kulipa kodi bila kubughudhiwa na hatimae kuongeza pato la taifa na kuepuka kuendesha miradi kwa fedha za wahisani ambazo zinakua na masharti magumu.

Bi. Ashantu ameongeza kuwa wabunge watambue kuwa hatua hizo zinazochukulwa na serikali ya awamu ya tano chini ya Uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli na muhimu hivyo kuwaomba wabunge hao wamuunge Mkono.

Sauti ya Naibu wa Fedha na Mipango Mhe. Ashantu Kijaji