Mbunge wa Singida Mashariki ambae pia ni Mwanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Tundu Lissu
Juzi asubuhi alifika Mahakamani kuitikia wito wa kwenda kujibu tuhuma za uchochezi zinazomkabili ambapo kesi yake iliahirishwa hadi Julai 11 mwaka huu lakini hapo jana Mhe. Tundu Lissu aliitwa tena kuhojiwa na jeshi la polisi.
Lissu aliingia jana aliingia kituo cha Polisi cha kati Jijini Dar es Salaam, majira ya Saa saba na nusu mchana kwa ajili ya kuhojiwa na ilipofika saa kumi na nusu jioni wakili wake alijitokeza mbele ya waandishi wa habari na kusema mteja wake huyo amenyimwa dhamana.
Kwa upande wake Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, alifanunua kile kilichopelekea Mhe. Tundu Lissu ambae pia ni Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria bungeni kuhojiwa na kueleza kuwa ni kutokana na kauli yake aliyoitoa mara baada ya kuhojiwa juzi mchana.