
Zitto Kabwe
Zitto ametoa rai kwa watekaji kwamba wamuachie Raphael kwani hana taarifa zozote zinazomhusu yeye, kwani aliacha kufanya kazi na Raphael miaka mitatu iliyopita na kudai kuwa, masuala ya utekaji ni ushamba hivyo wamuachie akajiunge na familia yake.
''Tuwaombe tu watekaji wamuachie maana hana taarifa zozote, na kosa kubwa walilolifanya watekaji ni kuanza kuutumia ukurasa wangu kuandika mambo yanayomsifia Magufuli, hiyo inamaana kwamba wanaomuunga mkono Magufuli ndiyo watekaji'', amesema.
Aidha Zitto ameongeza kuwa, wao kama marafiki wa Raphael wamefanikiwa kupata hadi mahali alikowekwa baada ya kutekwa, na baadhi ya taarifa wamewapa polisi na kwamba wanajua walipomuweka kuanzia siku ya kwanza hadi Jumamosi.
''Niwaombe watekaji wasifanye mambo yoyote ya kijinga kwani gharama yake ni kubwa, wamuache kokote sisi tutaenda kumchukua''.
Zitto amesema masuala ya utekaji hayaleti taswira nzuri kwa nchi na nchi jirani, na kwamba vyombo vya usalama vya Taifa vimekuwa vikihusishwa na masuala haya kitu ambacho ni aibu, na hivyo ni vyema watoke wajisafishe kwa jamii na kwamba itafikia hatua watekaji na wao wataanza kutekwa.