Jumatano , 13th Jul , 2022

Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge, amewataka wananchi kushirikiana na serikali kukabiliana na vitendo vya uvuvi haramu ambavyo vinachangia kuathiri uchumi wa mkoa kutokana na kuharibu rasilimali za ziwa Victoria ambalo ni chanzo cha mapato kwa wananchi na serikali.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali, Charles Mbuge

Akizungumza katika eneo la Magarini wakati wa kukabidhi boti kwa ajili ya kufanyia doria katika ziwa Victoria upande wa wilaya ya Muleba, Mkuu wa mkoa huo Meja Jenerali Charles Mbuge amesema kuwa serikali ya awamu ya sita haiko tayari kuona vitendo hivyo haramu vinaendelea katika ziwa hilo.

"Na ndiyo maana tumechoma nyavu zenye thamani ya shilingi bilioni mbili, kwahiyo hizo ni salamu zilizopelekwa kwa wale wanaovua samaki kwa kutumia nyavu zisizofaa, lazima kila mmoja wetu alinde maliasili za Watanzania," amesema Meja Jenerali Mbuge.