Alhamisi , 14th Apr , 2022

Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyotolewa hivi karibuni imekuwa na ubadhilifu mkubwa huku akisema hayo ni madhara ya serikali kuendeshwa gizani.

Zitto Kabwe ametoa kauli hiyo wakati chama cha ACT Wazalendo kikifanya uchambuzi wa ripoti hiyo mbele ya wanahabari.

"Huko nyuma kumekuwa na taarifa kama hizi lakini Mimi nimekaa bungeni miaka 15, sijawahi kuona taarifa ya CAG ambayo ina wizi wa wazi wazi kama hii, na haya ni madhara ya kuendesha serikali gizani"

"Tuliaminishwa kuwa hakuna ubadhilifu, mambo yanakwenda sawa sawa, kila kitu ni kizuri lakini kumbe ni kwa sababu vyombo vya habari vilifungwa,bunge likawa gizani, wabunge waliokuwa  huru wakafukuzwa bila kufuata taratibu, kamati za bunge zikawa haziwezi kufanya chochote" amesema Zitto Kabwe

Kiongozi huyo amesema kwa sasa watu wameanza kuwa huru na ndio maana watu wanaijadili ripoti hiyo vikiwemo vyombo vya habari na wadau mbalimbali