Ijumaa , 1st Mei , 2015

Shirikisho la vyama vya wafanyakazi mkoa wa Dar es salaam wamemtaka Rais Jakaya Kikwete awasaidie wapunguziwe kodi kubwa wanazolipa wafanyakazi hapa nchini huku wakitaka wafanyabiashara nao walipe kodi kama wafanyakazi.

Gratian Mukoba, Rais mpya wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA).

Msimamo huo wa TUCTA, mkoa wa Dar es salaam umesomwa na mratibu wa TAMCHO Charles Mgashi wakati akisoma hotuba yao mbele ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ambaye ndiyo mgeni rasmi katika siku ya wafanyakazi mkoa wa Dar es salaam yaliyofanyika katika uwanja wa uhuru.

TUCTA wametaka pia mishahara iongezwe mpaka 720,000 kima cha chini toka laki mbili na nusu za sasa ambazo hazitoshi huku wakilalamikia kodi nyingi pamoja na makato hata katika mafao yao pindi wakistaafu na hivyo kuwarudisha nyuma badala ya kuwasaidia pindi wanapostaafu.

Kwa upande wa serikali kupitia mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mecky Sadick amesema kuwa atalifikisha kwa Rais ili atolee majibu ya madai hayo ya wafanyakazi ya muda mrefu.

Kuhusu mishahara tamko litatolewa na mawaziri wa kazi na utumishi wa umma katika bunge la bajeti baada wiki ijayo.