Rais mteule wa Marekani, Donald Trump.
Kulingana na timu ya mpito ya Trump, viongozi hao wawili walizungumzia uchumi, siasa pamoja na masuala ya kiusalama.
Mazungumzo hayo ni ya kwanza ya aina kutokea kati ya Marekani na Taiwan tokea mwaka 1979.
China inakataa kuitambua Taiwan kama taifa huru na inapinga mahusiano yoyote yaliyo rasmi na taifa hilo, huku hadhi ya kisiwa hicho imekuwa kwa muda mrefu moja ya masuala yenye utata zaidi kati ya Marekani na China.
Trump ameonyesha kukosa diplomasia katika masuala yanayoihusu China, huku Rais wa Taiwan akiapa kuwa katu hatokubali shinikizo la China.







