
Akiongea mara baada ya kuzindua mpango huo kwa niaba ya Katibu kiongozi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome amesema kuwa mpango huo wa miaka mitano kuanzia 2016-2010 kipaumbele kimewekwa katika maeneo 12 ikiwa ni pamoja na masuala ya utawala bora, haki za binaadamu na masuala ya kijinsia.
Aidha, katika mpango huo wa maendeleo wa miaka mitano jumla ya fedha za kitanzania shilingi trilioni 2.8 zimetengwa kutumika ambapo asilimia 8 ya fedha hizo itakuwa ni kwa ajili ya Zanzibar.
Kwa upande wake Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bw. Alvaro Rodriguez amesema kuwa mpango huo unazindiuliwa ukiwa na kauli mbiu “pinguza pengo ili kutomwacha nyuma mtu yoyote “ Unamtaka kila Mtanzania kufanya kazi kwa bidii ili kuyafikia kikamilifu malengo endelevu ya dunia.