Ijumaa , 23rd Sep , 2022

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete, amesema kwamba Treni ya umeme kutoka Dar es Salaam, hadi Morogoro itaanza kufanya kazi rasmi mwezi Februari 2023, kwani vichwa vya Treni, mabehewa ya abiria na mizigo yanatarajiwa kufika nchini mwezi Novemba.

Treni ya umeme

Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 23, 2022, Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum Dkt. Christine Ishengoma lililohoji ni lina sasa Treni hiyo itaanza kufanya kazi.

Ambapo katika jibu lake Naibu Waziri Mwakibete amesema, "Matarajio yetu reli ya SGR ingeanza Septemba hii lakini kutokana na changamoto ya usafirishaji wa vipuli na mabehewa kulikuwa na changamoto ya kupata Meli kutoka Ujerumani, habari njema ni kwamba tayari vichwa vya Treni, mabehewa ya abiria na mizigo vimekwishapakiwa kwenye Meli kuja nchini, Novemba vitafika na tutafanya majaribio mpaka Januari hivyo Februari 2022, SGR kutoka Dar kuja Morogoro itaanza rasmi,".