Jumapili , 14th Feb , 2016

Mamlaka ya mapato nchini Tanzania (TRA) imewataka watanzania kuisaidia nchi kupiga hatua ya kimaendeleo kwa kujitokeza kulipa kodi na kuhalalisha shughuli wanazozifanya kwa kushirikiana na mamlaka hiyo.

Mkurugenzi wa Huduma na elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Bw. Richard Kayombo

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA Bw. Richard Kayombo, amesema hayo wakati akiongea na kikundi cha washereheshaji, wapishi na waandaaji wa sherehe kuhusu kujirasimisha ili kuingia rasmi katika mfumo wa ulipaji kodi.

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wamesema moyo wa kuitumikia nchi ndio uliowafanya kuomba elimu itakayowawezesha waanze kulipa kodi, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo mapato ya shughuli zao yalikuwa hayalipiwi kodi.

Imebainika kuwa Wajasiriamali wengi hawamo katika orodha ya ulipaji kodi kutokana na shughuli zao kutokutambuliwa na Mamlaka hiyo hivyo kulikosesha taifa mapato kutokana na shughuli hizo nyingi zikiwa zinawaingizia wajasiriamali hao pato kubwa.