Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati wa utoaji wa tuzo za Rais John Pombe Magufuli kwa wazalishaji bora wa bidhaa kwa mwaka 2018, zinazotolewa na Shirikisho la viwanda nchini (Cti).
''Haiwezekani mtu hata kunywa juice, zinazozalishwa na viwanda vya ndani ukawa hautaki, unataka zile zilizotengenezwa nje, huwezi kuvaa kiatu kutoka nje wakati hata hapa tunavyo, hata mimi hapa nimevaa kiatu kilichotengenezwa hapa nchini ni lazima watanzania tuwe na utaratibu wa kupenda bidhaa zetu'' amesema Waziri Mkuu.
Aidha Waziri Mkuu ameongeza kuwa, Serikali imeendelea kuimarisha ulinzi ili kudhibiti uingizwaji holela wa bidhaa za nje kupitia bandari bubu zilizopo hapa nchini

