Taasisi ya Uangalizi wa Uchaguzi nchini Tanzania (TEMCO) imesema zoezi la uandikishaji wananchi katika daftari la kudumu wapiga kura kwa mfumo wa BVR limeonesha kushindwa kufanikiwa kutokana na baadhi ya maeneo kuandikisha wahamiaji haramu, pamoja na wananchi wasiokidhi vigezo vya kupiga kura.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa tathmini ya awali ya namna zoezi hilo lilivyofanyika meneja wa mradi wa (TEMCO) Dk. Benson Bana amesema zoezi hilo pia lilistahili kushirikishwa wafungwa wanatotumikia kifungo cha miezi sita kama sheria inavyoelekeza lakini imekuwa ni tofauti.
Dkt. Bana amesema wananchi wengine wameshindwa kuandikishwa kutokana na uelewa duni wa elimu ya uraia katika uandikishwaji wapiga kura kwa mfumo wa BVR na hivyo kupoteza haki yao ya kupiga kura.

