Jumamosi , 2nd Jul , 2022

Tembo wamevamia na kuvunja nyumba tano katika Kijiji cha Ming'ongwa, Kata ya Sakasaka, wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, leo Julai 2, 2022.

Moja ya nyumba ambazo zimebomolewa na Tembo

Diwani wa Kata ya Sakasaka, Emmanuel Maliganya, ameiambia EATV kuwa Tembo hao wameharibu pia mashamba ya denge, katika Kijiji hicho

"Pia,Tembo wamevamia familia ya Ng'wandu Jisinza na wakalikimbiza dume la Ng'ombe na walipolipata wakalikanyaga kanyaga na kulichoma tembe hadi kufa," amesema Diwani Maliganya.