Jumapili , 30th Mar , 2014

Chama cha wamiliki wa malori nchini Tanzania TATOA, kimetoa magari matatu na pikipiki 20 kwa ajili ya kukabiliana na uporaji na wizi unaofanywa kwenye malori yanayosafiri katika barabara kuu nchini.

Msemaji wa chama cha wamiliki na wasafirishaji wa malori nchini Tanzania TATOA, Bw. Elias Lukumay.

Mwenyekiti wa TATOA Bw. Seif Ally amesema utekaji huo umesababisha baadhi ya wafanyabiashara kuacha kutumia bandari ya Dar es Salaam kwa hofu ya mizigo yao kuporwa ikiwa njiani.

Seif amesema vifaa hivyo vyenye thamani ya fedha za Tanzania shilingi milioni 315, vimetolewa kwa jeshi la polisi ili liimarishe doria katika barabara kuu nchini, na kupunguza matukio ya uporaji wa shehena ya mizigo ambayo hivi sasa yanaonekana kushamiri.