Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli
Rais Magufuli ameyabinisha hayo leo Machi 13, 2020, wakati wa uzinduzi wa karakana ya kutengeneza magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), katika kambi ya jeshi hilo maeneo ya Lugalo Jijini Dar es Salaam na kuwaomba wananchi waache kusafiri safiri hovyo.
"Nimetoa maagizo kwa Katibu Mkuu kiongozi, hatutatoa vibali vya watu kusafiri safiri kama wanavyotaka, tatizo hili lipo, tahadhari tunazopewa tusizipuuze, tusishikane mikono, tusibusiane, sasa hata usiku sijui itakuwaje, lakini unaweza ukakwepa na mambo yakawezekana na miraha tu" amesema Rais Dkt Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amewasisitiza wananchi kuhakikisha wanazingatia tahadhari zinazotolewa kwa kuwa ugonjwa huo ni hatari kwani hata dawa yake haipo na kwamba ugonjwa huo unarudisha uchumi nyuma.







