Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Moremi Marwa
Hayo yamesemwa leo Septemba 30, 2019 jijini Dar es salaam na Afisa mtendaji mkuu wa soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) Moremi Marwa, ambapo amesema fursa hiyo itasaidia kuongeza idadi zaidi ya wawekezaji wa ndani na nje hivyo kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
“Sisi kuingia katika nafasi hii inatufanya kuwa katika ile orodha ya vitabu vya uwekezaji ni jambo kubwa kwasababu tunategemea itaongeza ukwasi sokoni na itawafanya hawa wawekezaji wakubwa na hata wadogo kujiamini zaidi”, amesema Marwa.
Aidha kwa mujibu wa taarifa ya mwenendo wa soko kwa juma lililoishia Septemba 27, 2019 imeonesha kuwa thamani ya soko la hisa imeshuka kutoka Trilioni 19.03 hadi kufikia Trilioni 19.01.




