Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dr. Seif Rashid
Akiongea kwa Niaba ya Waziri wa Afya Dr Seif Rashid naibu mkurugenzi wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Ayubu Magimba amesema idadi ya wagonjwa wa Seli Mundu huongezeka kila mwaka kwasababu ya jamii kutopenda kupima afya zao mara kwa mara haswa ugonjwa wa Seli Mumbu na hivyo kushindwa kuudhibiti mapema kama wangejua kuwa wana vinasaba vya ugonjwa huo.
Dr Magimba ameongeza kuwa mpango wa kudhibiti ugonjwa huu umesaidia sana katika kuwatambua watoto wenye dalili za ugonjwa huo na kuwapa matibabu sahihi ili kuudhibiti mapema na kuitaka jamii kupunguza unyanyapaa kwa watu wenye ugonjwa huo.
Aidha Dr Magimba amesema kuwa watu wenye ugonjwa huo huishi miaka mingi kama wakigunduliwa mapema na kupata matibabu sahihi.