Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana
Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana, Jijini Dodoma wakati akizindua mpango kazi wa Kitaifa wa usimamizi shirikishi wa misitu na takwimu za usimamizi shirikishi wa misitu ya jamii, na kuwataka wadau wa misitu nchini kusoma kwa makini takwimu za usimamizi shirikishi wa misitu ili kupata picha ya hali halisi.
"Ili nyaraka hizi zieleweke vyema na kutumika kwa ukamilifu miongoni mwa wadau walio wengi, ninaiagiza idara ya misitu na Nyuki izifanyie tafsiri nyaraka hizi ziwe kwa lugha ya Kiswahili na zisambazwe kwa wadau wengi kwa kadri itakavyowezekana" amesema Balozi Chana
Aidha, amewahimiza wamiliki wa misitu ya jamii ikiwemo ya vijiji kuisimamia kikamilifu kulingana na sheria, kanuni na miongozo iliyopo akisisitiza kuwa iwapo mpangokazi aliouzindua utatekelezwa ipasavyo, utawezesha uhifadhi na matumizi endelevu misitu ya jamii na pia kuchangia maendeleo endelevu katika sekta nyingine.


