Afisa Masoko na elimu kwa umma wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Bw. Rajabu Mwenda (kulia) akizungumza na waandishi w habari katika ofisi za mpango huo hivi karibuni.
Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wa Mapango huo Bw Rajab Mwenda amesema hayo leo wakati akitoa takwimu za kiwango cha damu kilichokusanywa kwa kipindi cha miezi mitatu iliyoishia Juni mwaka huu ambapo katika kipindi hicho mpango umekaribia lengo kwa kukusanya asilimia 91 ya lengo.
Akizungumzia usalama wa damu wanayokusanya, Bw. Mwenda amesema asilimia 5.6 ya damu yote waliyokusanya katika kipindi hicho imebainika kuwa na maambukizi ya ugonjwa hatari wa homa ya ini, huku ile yenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI ikiwa ni asilimia 1.6.
Katika hatua nyingine, kutopimwa magonjwa ya moyo kwa watoto wachanga mara tu wanapozaliwa katika hospitali mbalimbali nchini Tanzania kumeelezwa kuchangia kwa kiasi kikubwa watoto kupoteza maisha kwa magonjwa hayo kutokana na wazazi wengi kutofahamu dalili zinazoashiria watoto kusumbuliwa na magonjwa hayo.
Wakiongea na East Africa Radio Wazazi wa watoto waliojitokeza kuwapima watoto wao magonjwa ya moyo na kubainika kuwa na magonjwa hayo ili kusaidiwa kwenda kutibiwa nchini India katika hospitali ya Regency wamesema wamehangaika na watoto wao pasipo kujua nini kinawasumbua kwa muda mrefu.
Kwa upande wake, Daktari Khuzema Khanbhai amesema wameamua kuwapima watoto wachanga wenye umri wa siku moja hadi miaka 18 ambapo wengi wa watoto waliowapima wamebainika kuwa na matundu kwenye moyo.