Jumapili , 31st Jul , 2016

Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shegela amewataka wakazi wa mkoa huo kutumia nafasi za ujio wa bomba kubwa la mafuta kutoka oima nchini Uganda hadi bandari ya tanga iliyopo mkoani humo kwa kuwekeza katika uzalishaji wa vyakula

na makazi ambayo yatatumiwa na wageni watakao fika kwa ajili ya ujenzi.

Akizungumza jijini Dar es salaamu wakati wasemina ya wakuu wa mikoa mheshiwa SHEGERA amesema ujenzi wa bomba hilo utakuja na nafasi nyingi za kibishara hivyo wakazi wa tanga ni muhimu wakatumia ujio wa mradi huo wa kujipatia kipato kwa kuwekeza katika uzalishaji wa vyakula kwa wingi na ujenzi wa hoteli kubwa zitakazo tumiwa kwa ajili ya malazi kwa wajenzi na wageni wengine.

Aidha Mheshimiwa SHEGERA amebainisha kuwa kwa sasa mkoa huo umejikita katika mambo matano yatakayo fanikisha mradi wa bomba hilo la mafuta ambapo wamejikita katika kuboresha bandari itakayo tumiwa kuhifadhiwa mizigo ,ujenzi wa tenki farm kwa ajili ya kuhifadhia mafuta ghafi ,ujenzi wa sehemu ya kuhifadhia vifaa vya ujenzi wa bomba hilo ,na ardhi ambayo itatumika kwa ajili ya kupitisha bomba hilo .