Alhamisi , 28th Aug , 2014

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini Tanzania (TAMWA) kimezilaumu taasisi za kidini na asasi zisizo za serikali kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo kuzuia vitendo vya ukatili kwa watoto.

Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA Bi. Valerie Msoka.

Lawama hizo zimetolewa licha ya taasisi hizo kuhamasisha masuala yanayohusu malezi na haki ya mtoto kuhakikisha yanapewa kipaumbele dhidi ya mkingano wa sheria na kusababisha kuongezeka kwa matukio ya ukatili kwa watoto.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa chama hicho Gladness Munuo, amesema upo umuhimu wa kuzipitia upya sheria za nchi na kuzifanyia marekebisho sheria zinazomlinda mtoto hasa ile inayotaja umri halisi wa mtoto wa kike kuolewa.

Kwa mujibu wa Munuo, mabadiliko ya sera za kisiasa na kiuchumi yameathiri namna taasisi za kijadi na za kidini zinavyofanya kazi, huku mzigo mkubwa wa malezi ukiachiwa serikali na wengine kujihisi hawahusiki na watoto hivyo kukosa sera zinazowatetea watoto.