Jumatano , 5th Aug , 2015

Takwimu ya ajali za barabarani kitaifa zimeonyesha kupungua kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia kipindi cha miezi sita ya mwaka 2015 tofauti na miezi sita ya mwaka 2014.

Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani nchini, Mohamed Mpinga.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani nchini, Mohamed Mpinga katika baraza la Taifa la usalama barabarani kwenye mkutano wa mkuu wa wadau wa usalama barabarani uliofanyika katika ukumbi wa regal naivera jijini hapa.

Kamanda Mpinga amesema takwimu za ajali zilizotokea kwa kipindi cha miezi sita ya mwaka 2014 na mwaka 2015 zinaonyesha kuwa kuna upungufu wa majeruhi pamoja na vifo vilivyotokana na ajali hizo za barabarani.

Kwa upande wake Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Tanga Abdi Isango amesema anategemea wananchi wataelimika kupitia vyombo vya habari mbalimbali nchini na watabadilika kutoka kwenye wimbi kubwa la ajali kwa kufuata matumizi sahihi ya barabara.

Nae Iddi Azan ambae ni mjumbe wa bodi hiyo pia ni mbunge wa jimbo la kinondoni amewataka madereva na watumiaji wote wa vyombo vya moto kujifunza na kuzielewa sheria za usalama barabarani ili kujikinga na kukomesha ajali hizo mbali na visingizio vya kusema barabara ni mbovu.