Jumatano , 21st Nov , 2018

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza inamshikilia mmoja ya watumishi wa idara ya uchumi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kaswalala Benjamini Elisha kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya shilingi laki tatu kutoka kwa mfanyabiashara.

TAKUKURU Makao Makuu

Akiongea na waandishi wa habari, Jijini humo Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Emanuel Stenga amesema mtuhumiwa huyo akiwa na mwenzake waliomba hela kwa mfanyabiashara wa vifaa vya maabara za shule za sekondari wakijifanya ni maafisa usalama wa taifa.

Aidha Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza Emmanuel Stenga amebainisha kuwa taasisi inaendelea kumtafuta moja ya watuhumiwa waliokuwa wameambatana na mchumi huyo ili wafikishwe mahakamani kwa kujibu mashtaka yao.

Mapema leo Kamanda wa Polisi Jijini humo alikanusha juu ya uvumi wa kuwepo kwa mgomo wa wafanyabiashara wa soko la Mlango mmoja kwaka kile kilichosemekana kuwa kutopewa kibali cha kujenga vibanda vyao ambavyo vilivyoharibiwa.

Bonyeza Link hapo chini kupata alichozungumza Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza Emmanuel Stenga