Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

TAKUKURU yaahidi kutoa milioni 10

Jumanne , 14th Nov , 2017

Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) yaahidi kutoa donge nono la milioni 10 kwa mtu yeyeote atakayetoa taarifa mahali alipo aliyekuwa mtumishi wa taasisi hiyio Bwana Godfrey John Gugai ambaye wanamtafuta kwa kuwa na mali nyingi.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari leo Naibu Mkurugenzi wa TAKUKURU  Brigadier General John Mbungo amesema mtu huyo awali alianza kuonyesha ushirikiano walipoanza kumuhoji, lakini baada ya muda akaanza kuwakwepa na hatimaye kutokomea kusikojulikana.

"Tumeendelea kumtafuta na taarifa tulizozipata amekuwa anakimbia nchi kupitia njia ambazo sio rasmi na hadi sasa tumeendelea kumtafuta lakini bado hajapatikana. Na sisi tumeona ni vema tuziweke hizi habari ziwe wazi kwenu waandishi wa habari na wananchi, popote watakapompata au kumuona huyu bwana watoe taarifa katika chombo hiki na taasisi hiii itamzawadia mtu yeyote ambaye atafanikisha kupatikana kwa huyu mtu, zawadi ya milioni 10 pesa taslim.", amesema Brigadia Mbungo.

Godfrey Gugai alikuwa mhasibu wa TAKUKURU anatuhumiwa kuwa na mali nyingi kinyume na sheria kwa mtumishi wa umma, ambapo ana nyumba ya ghorofa 4 iliyopo Ununio Knondoni, nyumba ya ghorofa 3 Bunju, ana nyumba za kupangishwa Mbweni, ana nyumba za kupangisha Kinondoni, ana jengo la kifahari Majita Musoma, ana nyumba Mwanza, ana nyumba ya kifahari Mwanza Nyegezi, ana viwanja lukuki sehemu mbali mbali na mali nyinginezo.

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali