
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samuel Sitta enzi za Uhai wake alipokwenda kumjulia hali nyumbani kwake Mbezi Dar es Salaam
Mhe. Samweli Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Tecknical Univesirty of Munich nchini Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu tangu mwezi uliopita.
Katika Salamu hizo Rais Magufuli amesema kuwa amepokea kifo cha Mh. Samweli Sitta kwa mshtuko na masikitiko makubwa na kwamba taifa limepoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika uongozi na maendeleo.
“Namkumbuka mzee Sitta kwa uchapakazi wake, uzalendo wake na tabia yake ya kusimamia ukweli katika kipindi chote alichokuwa katika ngazi mbalimbali za kisiasa na serikali”
Rais Dkt. Magufuli amesema anaungana na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha maombelezo na amewaombea moyo wa uvumilifu na ustahimilivu.
Katika hatua nyingine, Bunge limesitisha vikao vyake vilivyokuwa vikiendelea mjini Dodoma hadi kesho kwa ajili ya kuomboleza msiba huo.