Jumatano , 23rd Nov , 2022

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, amesema kwamba serikali bado haijatoa taarifa ya uchunguzi wa ajali ya ndege ya Presicion Air iliyotokea Novemba 6, 2022, hivyo taarifa inayosambaa mitandaoni ipuuzwe kwani haijatolewa na mamlaka rasmi za serikali.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa

Taarifa hiyo ameitoa hii leoe Novemba 23, 2022, kupitia ukurasa wake wa Twitter na kusema kwamba taarifa kamili itakapokuwa tayari wananchi watajulishwa.