
Akizungumza na viongozi wa Jeshi la Jadi Sungusungu Tarafa ya Shinyanga Mjini,Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amesema yamekuwa yakitokea matukio ya uhalifu ikiwemo watu kukatwa mapanga na kuchomwa visu huku jeshi la sungusungu lipo maeneo hayo na kuwataka kuwa wakali ili kukomesha vitendo hivyo.
Kwa upande wake Kamanda Mkuu wa Sungusungu Manispaa ya Shinyanga John Kadama amesema wamejipanga kuhakikisha wanakomesha matukio ya uhalifu.
Nao baadhi ya washiriki wa kikao hicho wakaeleza namna ambavyo watakwenda kudhibi matukio ya uhalifu kwenye maeneo yao.