Jumatano , 29th Apr , 2020

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa, ofisi yake itajitahidi kwamba mpaka kesho jioni Mbunge wa Sumve Richard Ndassa, aliyefariki Dunia mapema leo anazikwa nyumbani kwao.

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai

Spika Ndugai ameyabainisha hayo wakati akiahirisha Mkutano wa 19, Kikao cha 9, cha Bunge hadi kesho Aprili 30, na kusema kuwa Mila za Kiafrika ni ngumu kumzika mtu popote pale isipokuwa nyumbani kwake.

"Tutajitahidi sana iwezekanavyo kuhakikisha kwamba huyu ndugu yetu anazikwa kule Sumve kesho jioni kwa Mila zetu za Kiafrika, kiukweli kumzika mtu popote pale ni jambo linalotuwia ugumu sana, fikiri yeyote uliyepo hapo upatwe na jambo hilo halafu uwekwe popote ni ngumu sana , Ofisi yangu tutashirikiana na Serikali kuona kile kinachowezekana kinafanyika" amesema Spika Ndugai.

Mbunge Richard Ndassa amezaliwa Machi 1959 na ameanza kulitumikia Bunge la Tanzania kuanzia mwaka 1995, na amekuwa Mbunge wa Sumve kwa vipindi vitano mfululizo.