Ijumaa , 15th Mei , 2020

Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, ameikataa Hotuba ya Wizara ya Fedha kutoka Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, kwa kile alichokidai kuwa hotuba hiyo imeandaliwa na Mbunge ambaye hayupo ndani ya Bunge hilo.

Salima Mdee Mbunge wa Kawe na Spika Ndugai

Kupitia vikao vya Bunge ambavyo ameviendesha leo Mei 15, 2020, Bungeni jijini Dodoma Spika Ndugai ameendelea kusema kuwa, hajaikubali hotuba hiyo kwa kuwa mwandishi wa hotuba hiyo ni Mbunge Halima Mdee na hayupo ndani ya Bunge.

"Hotuba ya kambi rasmi hatujaikubali sababu mwandishi wake ni Halima Mdee ni kati ya wale waliojifukuza wenyewe Bungeni, kwamba roho zao ni muhimu kuliko wengine, haiwezekani ukapitishia dirishani kazi zako zikafanyika, wakati wewe hata uliko hakujulikani" amesema Spika Ndugai

Mapema leo Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, alitoa waraka juu ya kuwataka Wabunge wake ambao walitekeleza agizo la kukaa Karantini kwa siku 14 warejee Bungeni kuanzia leo.