
Lema ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya ndani ameyasema hayo katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha ITV jijini Dar es salaam.
‘’Kila mtu sasa hivi yupo kwenye pilika pilika kuanzia wabunge na kila mtu hakuna anayejali watoto tena watoto tumewaachia wafanyakazi pamoja na runinga kila siku hii ni athari kubwa sana katika kizazi chetu’’ Amesema Lema.
Kuhusu wabunge kutumia vilevi Lema amesema huko ndiko kuporomoka kwa maadili ambako hata kwa upande wa Bunge kuna ukiukwaji mkubwa wa kanuni ndiyo maana askari huingia ndani ya bunge hilo na kuwakamata wabunge hadi wengine kuchaniwa nguo huku serikali ikitizama hali hiyo na kuwa kimnya.
Aidha Lema amesema Rais Magufuli kuna baadhi ya mambo anafanya vizuri katika kuleta heshma ya nchi lakini kama mambo anayofanya yasipowekwa kisheria akiingia mtu mwingine ataanza na mambo yake kama ilivyofanyika kwa awamu zilizopita.