
Kufuatia tukio hilo kamati ya ulinzi na usalama imelazimika kufika kijijini hapo ikiongozwa na Claudia Kitta ambaye ni mkuu wa wilaya na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ambapo anakiri kutokea kwa tukio hilo na kutoa rai kwa wananchi kutotembea usiku kipindi ambacho wanyama hao wakali wanatafutwa.
Kwa upande wake ofisa wanyama pori hifadhi ya Mpanga Kipengere Diminick Rwebangira ametoa pole kwa waliyoathiriwa na uvamizi wa wanyama hao na kuwataka kuchukua tahadhali