Jumatatu , 19th Jun , 2023

Simba waliotoka katika hifadhi ya Ruaha wamevamia vijiji vya Magunga, Kiponzero na Makongati mkoani Iringa na kula Ng’ombe 13, Nguruwe 1 na kuku mmoja ikiwa ni siku ya tano hadi leo na Simba hao bado hawajadhibitiwa

Akizungumza na East Africa Radio Mkuu wa hifadhi ya Ruaha Godwell Ole Meing’ataki amesema bado wanaendelea na juhudi za kuhakikisha wanawakamata samba hao n akuwarudisha hifadhini

Kwa nyakati tofauti wanakijiji wa Magunda na Kiponzero Baraka Dalu na Freddy Mhavile wanasema kwa sasa wamekuwa na hofu sit u kwa ajili ya mifugo yao bali pia kuhusu usalama wa watu katika maeneo husika

 
Ripoti Kamili kuhusu habari hii sikiliza Supa Breakfast Kesho kuanzia saa 12 na nusu Asubuhi