Mbunge wa Viti Maalum kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Jesca Kishoa.
Jesca Kishoa ametoa kauli wakati akizungumza na www.eatv.tv ikiwa leo ni maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani ambayo huadhimishwa Machi 8 ya kila mwaka.
Kishoa amesema, "hii si mara ya kwanza mimi kutofautiana na mume wangu (David Kafulila) tulishawahi kutofautiana kwa sababu wakati ananichumbia mimi nilikua natokea kanisa la KKKT yeye alitokea Katoliki."
"Lakini pia tulitofautiana alipokuwa NCCR Mageuzi mimi nilikuwa CHADEMA, lakini sasa hivi tunatofautiana yeye yuko CCM, lakini tumekubaliana kutokukubaliana kwenye masuala ya kiitikadi lakini inapofika masuala ya familia lazima tuzungumze lugha moja", ameongeza Kishoa.
Kafulila ni miongoni mwa wanasiasa ambao walishawahi kuwa wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa nchini, ikiwemo NCCR Mageuzi, CHADEMA na baadaye alitangaza kuhamia CCM na kuteuliwa na Rais Magufuli kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Songwe.
