Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt Bashiru Ally.
Dkt Bashiru ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Mabalozi na viongozi wengine wa chama hicho, katika Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera.
"Kuabudu watu ni ushirikina, wanaotaka kutukuzwa na kujifanya wao ndio wanaweza mambo, wanafanya siasa za kishirikina" amesema Dkt Bashiru.
Aidha amewataka kuacha kufanyiana fitina ndani ya chama kwa kuwa fitina zina malipo yake, "Siwezi kuwazuia kunywa sumu kama mmeamua kufanya hivyo, lakini siwezi kuogopa kuongea ukweli" amesema Dkt Bashiru.

