Jumanne , 11th Aug , 2015

Chama cha ACT wazalendo kimewataka Watanzania kutodanganyika na sifa wanazovikwa baadhi ya wagombea wa urais katika kipindi hiki cha uchaguzi kwani baadhi yao wameshindwa kudhibiti wizi na ubadhirifu wa mali ya umma katika nyadhifa walizokuwa nazo.

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe akiwa anawahutubia wananchi wa Iringa katika uwanja wa mwembetogwa.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya mwembetogwa mjini iringa kiongozi wa chama hicho bwana zitto zuberi kabwe amesema kumekuwa na maneno mengi ya kuwapamba baadhi ya wagombea wa urais hasa UKAWA na CCM, lakini hakuna anayefahamu vyema uwezo wa wagombea hao katika kupambana na ufisadi hivyo.

Zitto ameongeza liwa Viongozi hao hawafai kupewa dhamana kubwa ya kuiongoza nchi kwakuwa hakuna jipya watakaloleta zaidi ya kuendeleza uporaji wa mali ya umma ni vema wananchi wakawa makini katika kuchagua kiongozi wao.

Nao makada wa chama cha ACT, waliohama kutoka CHADEMA, na kujiunga na chama hicho hivi karibuni chiku abwao na abuu changawa walipata tabu kuhutubia mkutano huo baada ya kukumbana na zomea zomea ya wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa chadema waliokuwa wakipinga hotuba zilizoonekana kuwashambulia viongozi wa chama chao.