Jumatano , 19th Mar , 2014

Shule za Msingi katika Kata ya Manzese Jijini Dar es Salaam zinakabiliwa na upungufu wa madawati na uchakavu wa miundombinu ya majengo hali inayohatarisha usalama wa wanafunzi wanaosoma katika shule hizo.

Afisa Elimu wa Kata hiyo Bi. Petronia Lyamuya amesema wanafunzi wamekuwa wakisoma katika mazingira hatarishi huku wakilazimika kukaa wanafunzi wanne mpaka sita katika dawati moja.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kilimani ambayo ni moja ya shule zilizopo katika Kata, Mwlimu Zubeda Jane amesema shule yake inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ya upungufu wa madawati 152.