Alhamisi , 15th Feb , 2024

Shule ya msingi Ludeba iliyopo kata ya Ipalamasa wilaya ya Chato mkoani Geita yenye wanafunzi zaidi ya 1500 inakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na vyoo vya kisasa Kwa walimu pamoja na wanafunzi wa shule hiyo.

Choo cha nyasi

Akizungumzia changamoto hiyo Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Daud William wakati wa ziara ya Mkuu wa wilaya ya Chato Deusdedith Katwale, alipotembelea katika katika shule hiyo amesema shule hiyo haina tundu hata moja la choo ambapo wanafunzi wamekuwa wakijisaidia kwenye choo cha nyasi kilichojengwa na wanafunzi wa kushirikiana na walimu baada ya vyoo vilivyokuwepo kutitia kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Mkuu wa wilaya ya Chato Mhandisi Deusdedith Katwale akiwa shuleni hapo aliwasiliana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Chato kwa njia ya simu na Mkurugenzi alisema tayari kuna fedha zimetengwa kwa ajili ya kunusuru wanafunzi wa Shule hiyo juu ya changamoto wanayoipitia.