Jumatano , 27th Mei , 2015

Chama cha Wamiliki wa vyombo vya habari nchini (MOAT) kimelalamikia Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari, na kusema kuwa iwapo muswada huo utapitishwa na kuwa sheria basi itakuwa ni sheria mbovu, yauonevu na yenye kukiuka Katiba ya nchi.

Mwenyekiti wa chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini Tanzania Dk. Reginald Mengi.

Akiongea leo wakati wa kutoa tamko la MOAT, kuhusina na muswada huo Mwenyekiti wa chama hicho Dk. Reginald Mengi amesema haki ya kupata habari ni haki ya kikatiba hivyo serikali haipaswi kuvunja Katiba ya nchi.

Aidha, Dk. Mengi amesema inashangaza kuona serikali kuingia katika mgogoro na vyombo vya habari katika wakati huu ambao taifa linaelekea katika uchaguzi mkuu, ambapo ilipaswa serikali na vyombo vya habari kuja pamoja kushirikiana.

Dkt. Mengi ameongeza kuwa haiwezekani kuwa na uchaguzi huru na wa haki kama utawanyima wananchi haki yao ya kupata habari na kusema kuwa vyombo vya habari ndivyo vinavyounganisha kati ya wananchi na serikali.

Amesema ni jambo lisilowezekana kutaka kukuza demokrasia kwa kudhibiti mambo ambayo yatakuza demekrasia pia kwa kupitisha sheria serikali itakua imekiuka katiba ya jamhuri ya Muungano yenye kubainisha kuwepo kwa uhuru wa kupata habari