Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo.
Mkuu wa Mkoa amelitoa kauli hiyo jana ,wakati alipozindua rasmi wiki ya nenda kwa usalama barabarani, ambayo kitaifa inafanyika Mkoani Arusha, mesema kuwa ajali nyingi zinatokana na uzembe huku watu wakijua kuwa kuwa sheria zilizopo sio kali.
Kwa upande wake akizungumzia malengo ya kuwa na wiki hii Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Pereira Ame Silima amesema yanalenga katika kuelimisha na kuwakumbusha watumiaji wa barabara katika kuzitumia barabara kwa usalama zaidi.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam katika maadhimisho ya ufunguzi wa wiki ya usalama barabarani, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana amelitaka jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kutoa elimu endelevu kwa wananchi wakiwemo wanafunzi ambao wengi wao ndio wameonekana kuathirika na ajali hizo.
Wakati huo huo, serikali ya Tanzania imezindua mpango maalum wa awamu ya pili wa kuendelezab sekta ya maji hapa nchini ambapo chini ya mpango huo maeneo yenye changamoto ya upatikanaaji wa maji yatapewa kipaumbele kutatuliwa changamoto hiyo kwa haraka.
Waziri wa Maji nchini Tanzania Prof: Jumanne Magembe amesema hayo wakati alipokuwa akizindua mpango huo huku akisisitiza upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo ya mijini na vijijini.
Amesema mpango wa uendelezaji wa sekta ya maji hapa nchini kupitia kwa wadau wa maendeleo utafanikisha kuwasaidia wananchi wa maeneo mbali mbali sasa kuwa na uwezo wa kupata maji tofauti na ilivyokuwa hapo awali.