Jumatano , 8th Oct , 2014

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ally Mohamed Shein aefuta uteuzi wa Mwanasheria mkuu wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, Othman Masoud Othman.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa jana, Rais Shein amefuta uteuzi huo kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo nchini ya kifungu cha 55 cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Kutokana na kumfuta kazi Mwanasheria huyo, Dkt. Shein amemteua aliekuwa naibu mwanasheria wa serikali hiyo Bw. Said Hassana Said kuwa mwanasheria mkuu wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.

Katika hatua nyingine, ukosefu wa maadili kwa viongozi wa kada mbalimbali nchini Tanzania kumetajwa kuwa ndio chanzo kikubwa cha kuporomoka kwa uchumi pamoja na kuendelea kwa vitendo vya ukatili baina ya wananchi.

Akiziungumza Jijini Arusha jana Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela ,kitivu Maadili na Falsafa Profesa Raymond Mosha, amesema kuwa kuongezeka kwa taarifa za matukio ya ukatili ikiwemo ubakaji,kuchomwa moto sehemu za mwili na mengine yakutisha na mfano halisi wa kuporomoka kwa maadili ya nchini.

Profesa Mosha, amesema kuwa ili kuweza kudhibiti hali hiyo ameiomba serikali kuanzisha mtaala wa elimu ya maadali kuweza kuanza kufundishwa kuanzia shule ya msingi hadi vyuoni ili kujenga viongozi wenye maadili ambao wataliletea taifa maendeleo.