
Waziri Nchemba ametoa ukanusho huo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya Makao Makuu ya Mambo ya Ndani jijini Dar es salaam.
Amesema serikali haipingani na dhehebu lolote nchi na kwamba pale ambapo kunakuwa na uhitaji wa kufanyia kazi jambo kuhusu taasisi hizo zilizopo chini ya wizara hiyo taratibu huwa zinatumika kuzungumza na sio kama ilivyofanywa kwenye taarifa hiyo inayosambaa.
Pamoja na hayo waziri huyo ameongeza "Serikali inalinda uhuru wa kuabudu na waumini hivyo taarifa hiyo inayosambaa ni batili na tayari uchunguzi umeanza kufanyika. Watu waache kuweka misimamo bila kuwa na uhakika wa taarifa kutoka serikalini ambao ndiyo wahusika wakutoa taarifa kisheria" .
Mbali na hato Waziri Nchemba ameonya wanasiasa wanaoingilia jambo hilo kisiasa kwa kusema kwamba kama umakini usipowekwa amani ya nchi itavurugika na ingawa bado wanaendelea na uchunguzi kuwabaini wahusika ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa.