
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe
Dkt. Mwakyembe amebainisha hayo bungeni pindi alipokuwa anajibu hoja ya mapendekezo ya bajeti ya Wizara ya ya Habari, utamaduni, sanaa na michezo ilichangiwa na Mbunge huyo kwa kutaka kufahamu ni kwanini serikali inawapuuza wadau wa masuala ya ubunifu (wasanii wa muziki na waigizaji ) hasa baada ya kuwatumia katika kampeni pamoja na chaguzi mbalimbali.
"Serikali haijawahi kuwapuuza wasanii nchini na kama nilivyosema katika hotuba yangu....Tumechukua hatua mbalimbali ya kuwajengea weledi, kuwakutanisha pamoja na kuwatambulisha na wadau wa maendeleo..Nitoe wito tu kwa baadhi ya vyama vya siasa ambavyo wanasiasa wao wanawachochea vijana kuimba nyimbo za kisiasa hii ni ‘entertainment industry’..Nilishawaambia vijana wangu wanipe mfano wa mwanamuziki yoyote duniani aliyefanikiwa kwa kuwatukana viongozi..Kama unataka siasa kagombea udiwani huko, kagombee nafasi yoyote huko hii ni ‘entertainment industry' na siyo 'Political industry'". Alisema Dkt Mwakyembe
Aidha, Dkt. Mwakyembe amewataka wasanii wote nchini kuboresha kazi zao ili waweze kutambulika duniani kama wasanii wenzao wa nchi za nje wanavyofanya nasiyo kuanza kuimba nyimbo zenye kutukana viongozi wao.